Kitengo cha zawadi na nadhiri kimeandaa zawadi za washiriki wa mahafali ya mabinti wa Alkafeel awamu ya nane

Kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa zawadi za kutabaruku kutoka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa washiriki wa mahafali ya mabinti wa Alkafeel awamu ya nane.

Zawadi zitatolewa kwa washiriki baada ya kukamilika vipengele vya mahafali ya wahitimu kwa wanafunzi wa vyuo kikuu vya Iraq na nchi za kiislamu (Mabinti wa Alkafeel) awamu ya nane.

Zawadi zinahusisha kipande za mswala uliopo ndani ya ukumbi wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya kusafishwa kwake.

Mahafali ya awamu ya nane inazaidi ya washiriki elfu 4 kutoka mikoa 15 ya Iraq na wanafunzi 170 kutoka nchi 7 za kiislamu ambazo ni (Kawait, Oman, Baharain, Saudia, Iran, Pakistani na Lebanon).

Mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq na nchi za kiislamu imeandaliwa na Idara ya shule za Alkafeel za wasichana chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, kauli mbiu inasema (Kutokana na nuru ya Fatuma –a.s) tunaangaza dunia) katika mwaka wa masomo 2023 / 2024.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: