Kuanza ratiba ya siku ya kwanza ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq na nchi ya kiislamu

Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza utekelezaji wa ratiba ya siku ya kwanza ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq na nchi za kiislamu awamu ya nane.

Mahafali imeandaliwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, kauli mbiu inasema (Kutokana na nuru ya Fatuma –a.s- tunaangaza dunia) kwa mwaka wa masomo 2023/2024.

Ratiba imekuwa na vipengele tofauti, miongoni mwake: Usomaji wa qaswida na mashairi ikiwemo hafla ya maadhimisho chini ya idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake.

Aidha kumekuwa na maonyesho yenye anuani isemayo (Sifa za uaminifu) yamesimamiwa na Bibi I’tidaal Daruweshi kutoka Oman, yameonyesha turathi za Oman na Khaliji yakiwa na ujumbe unaohimiza kushikamana na mwenendo wa kiislamu, na kufuata Ahlulbait (a.s) pamoja na kuhimiza hijabu.

Hali kadhalika kukawa na kipengele cha (Matonye ya unyweshaji) kilicho husisha mihadhara ya wanahabari na wahitimu wa awamu zilizopita, wameeleza uzowefu wao wa kushiriki kwenye mahafali ya mabinti wa Alkafeel, na namna ushiriki huo ulivyo athiri maisha yao ya kimasomo na kikazi.

Siku ya kwanza ikahitimishwa kwa kusoma qaswida maalum kutoka kwa washiriki zilizohimiza umoja na undugu wa kiislamu kwa wanafunzi.

Mahafali itaendelea kesho siku ya Ijumaa, kwa kufanya vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na utoaji wa zawadi na pongezi kwa wahitimu na kuwatakia mafanikio mema katika maisha ya kazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: