Balozi wa Italia nchini Iraq amepongeza huduma zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru na jamii.

Balozi wa Italia nchini Iraq muheshimiwa Nekolo Funtana, amepongeza huduma zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru na jamii.

Ametoa pongezi hizo alipotembelea Atabatu Abbasiyya na kukutana na makomo katibu mkuu Sayyid Abbasi Mussa Ahmadi, ambae ametoa maelezo kuhusu historia ya Atabatu Abbasiyya na huduma zinazotolewa kwa mazuwaru na jamii.

Fontana amesema “Atabatu Abbasiyya inatoa huduma kubwa kwa mazuwaru na jamii, jambo hilo linafaa kupongezwa, aidha mji wa Karbala unanafasi kubwa kiroho na kusambaza uislamu Iraq na dunia nzima kwa ujumla”.

Alipotembelea makumbusho ya Alkafeel iliyopo ndani ya Ataba tukufu, ameangalia mbinu za kutunza mali-kale, akasema kuwa “Makumbusho ni nzuri sana, inatumia mbinu bora zaidi ya kuonyesha mali-kale”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: