Idara ya Dini tawi la wanawake imetangaza ratiba ya vikao vyake vya usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani

Idara ya Dini tawi la wanawake chini ya ofiri ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza ratiba ya vikao vyake vya usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani.

Kiongozi wa idara Bibi Adhraa Shami amesema “Idara imeandaa ratiba maalum katika mwezi wa Ramadhani, yenye vipengele vingi ikiwemo vikao vya usomaji wa Qur’ani vitakavyo dumu mwezi mzima”.

Akaongeza kuwa “Idara itafanya vikao viwili vya usomaji wa Qur’ani kila siku, kutakuwa na kikao cha asubuhi na jioni ndani ya Sardabu ya Imamu Jawaad (a.s) iliyopo katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na vikao vingine zitafanywa katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f)”.

Akasema “Vikao vya usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani vinalenga kujenga utamaduni wa kufuata mafundisho ya vizito viwili katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: