Majmaa-Ilmi inapokea majaji wa mashindano ya kimataifa ya usomaji wa Qur’ani zawadi ya Al-Ameed awamu ya pili

Rais wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya Dokta Mustaqu Ali, amepokea majaji wa mashindano ya kimataifa ya usomaji wa Qur’ani tukufu awamu ya pili.

Washiriki wa mashindano hayo wanatoka katika nchi 53 za kiarabu na kiajemi, vijana wadogo na wakubwa.

Miongoni mwa aliowapokea rais wa Majmaa ni: Shekhe Muhammad Ahmadi Basiyuni, kutoka Misri, Ustadh Abdulkarim Haidari kutoka Afghanistan na kutoka Iraq amempokea Dokta Basim Abadi.

Tunatarajia kupokea wageni wote wanaokuja kushiriki kwenye mashindano haya ndani ya siku chache zijazo, kwa ajili ya kuanza ratiba ya mashindano.

Mashindano hayo ni sehemu ya mchango wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kusambaza utamaduni wa kusoma Qur’ani, ambayo ni msingi madhubuti wa kurekebisha mtu na jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: