Atabatu Abbasiyya tukufu imeratibu usomaji wa Qur’ani kwa wanafuni wa vyuo vikuu vya Iraq kupitia ratiba ya mabalozi wa ibada.
Msomaji wa Atabatu Abbasuyya tukufu Sayyid Muhammad Baaqir amesema “Ataba tukufu imeandaa ratiba ya usomaji wa Qur’ani kwa kushirikiana na Atabatu Askariyya kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq, kupitia ratiba ya mabalozi wa ibada inayoratibiwa na kitengo cha mahusiano”.
Akaongeza kuwa “Lengo la kuandaa ratiba ya usomaji wa Qur’ani ni kujenga utamaduni wa Dini kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na kuwahimiza kushikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu sambamba na kuwafundisha usomaji wa Qur’ani tukufu”.
Ratiba hii ni sehemu ya juhudi za Atabatu Abbasiyya za kueneza utamaduni wa kushikamana na mafundisho ya Qur’ani tukufu kwa watu wa tabaka tofauti katika jamii.












