Sayyid Sistani amepokea Daktari wa kiiraq Muhammad Abu Raghifu baada ya kurudi kwake kutoka Gaza.

Muheshimiwa Marjaa-Dini mkuu Sayyid Sistani, amepokea daktari wa kiiraq Muhammad Abu Raghifu Mussawi baada ya kurudi kutoka Gaza.

Tamko lililotolewa na ofisi ya Sayyid Sistali linasema “Marjaa-Dini mkuu Sayyid Ali Sistani amepokea Daktari wa kiiraq Muhammad Twahir Kaamil Abu Raghifu Mussawi na amesikiliza maelezo yake kuhusu hali ya kiafya katika mji wa Gaza”.

Tamko likaongeza kuwa “Sayyid Sistani amemshukuru daktari huyo kwa kazi kubwa aliyofanya kipindi chote cha uwepo wake Gaza”.

Muheshimiwa Sayyid Sistani amekuwa na msimamo wa wazi kuhusu yanayojiri katika mji wa Gaza na mateso wanayopata wapalestina, amekuwa akihimiza kusaidiwa watu wa Palestina, haki yao ya kijitawala, ulazima wa kusimama pamoja nao katika mitihani wanayopitia na kulaani ukatili wanaofanyiwa watu wa taifa hilo.

Ofisi ya Muheshimiwa Sayyid Sistani ilitoa tamko siku za nyuma kutokana na mateso ya watu wa Gaza lisemalo “Ulimwengu wote unadeni la kuzuwia unyama unaofanywa na jeshi la wavamizi dhidi ya watu wa Palestina wadhulumiwa”.

Akaongeza kuwa “Mateso ya watu hao –yamedumu kwa miongo saba- wanatakiwa kupewa haki yao na kumaliza uvamizi katika ardhi yao, ndio njia pekee ya kuleta Amani na usalama katika eneo hilo, bila kufanya hivyo mapigano yataendelea na watu wengi wasiokua na hatia wataendelea kuuawa”.

Msimamo wa Sayyid Sistani unaendana na misingi ya kibinaadamu, inayohitaji Amani na uadilifu, anahuzunishwa sana na yanayoendelea katika taifa la Palestina.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: