Kitengo cha habari kimeweka huduma ya uwasomea Qur’ani wanachuoni waliopita

Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya kupitia mtandao wa kimataifa Alkafeel, kinafanya huduma ya kusoma Qur’ani na kuelekeza thawabu zake kwa wanachuoni waliopita.

Kiongozi wa idara ya ufundi wa mitandandao chini ya kitengo, Sayyid Haidari Twalib Abdul-Amiir amesema “Idara ya mtandao wa kimataifa Alkafeel inatoa huduma ya kusoma Qur’ani na kuelekeza thawabu zake kwa wanachuoni waliopita ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Akaongeza kuwa “Tunatoa nafasi kwa msomaji kuchagua juzuu analopenda kusoma na kuelekeza thawabu za usomaji wake kwa mmoja wa wanachuoni, kila mwanachuoni kapangiwa siku maalum, kuanzia Shekhe Ali bun Ibrahim Alqummiy, aliyeishi katika zama za Imamu Ali Alhaadi (a.s), Shekhe Ali bun Hussein mzazi wa Shekhe Swaduqu na wanachuoni wengine, pamoja na kuelezea historia yao, vitabu walivyo andika na wanafunzi wao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: