Atabatu Abbasiyya inaendelea na vikao vya mwezi mtukufu wa Ramadhani

Atabatu Abbasiyya inaendelea na vikao vya mwezi mtukufu wa Ramadhani ndani ya ukumbi wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa siku ya pili mfululizo.

Idara ya wahadhidhiri katika Ataba tukufu, inaratibu vikao hivyo kupitia harakati zake katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mhadhiri wa kikao (majlisi) Sayyid Swadiqu Almurawiji amesema “Muhadhara niliotoa nimeongea kuhusu umuhimu wa kujitathimi na ulazima wa mtu kuangalia vitendo vyake na tabia yake, kwa lengo la kujipima na kujiboresha”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara umepata muitikio mkubwa, umepambwa na mifano ya kielimu na hadithi za Maimamu wa Ahlulbait (a.s)”.

Majlisi za mwezi mtukufu wa Ramadhani hufanywa mwezi mzima, ni sehemu ya kufundisha Dini na utamaduni wa kiislamu kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: