Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Allamah Sayyia Ahmadi Swafi, ametembelea kitengo cha malezi na elimu na kuangalia miladi yake mikuu.
Amepokewa na rais wa kitengo Dokta Daakhil Hasanawi, mkuu wa shule za Al-Ameed za wavulana Dokta Aadil Karkushi na mkuu wa shule za Al-Ameed za wasichana Bibi Mina Waail.
Katika ziara hiyo Sayyid Swafi ameangalia utendaji kazi wa kimalezi na kielimu, amepongeza mafanikio yaliyofikiwa chini ya mkakati wa kitengo cha malezi na elimu.
Sayyid Swafi amekagua miradi mikuu inayofaywa na kitengo, hususan mradi wa malezi na mbinu za kitengo katika kutekeleza mradi huo, amefurahishwa na kuahidi kusaidia jambo hilo, amewapongeza watumishi kwa kazi nzuri wanayofanya pamoja na idara zao.
Ziara hiyo ni sehemu ya uungaji mkono wake kwa kitengo cha malezi na elimu, kutokana na umuhimu wa kujenga kizazi cha watu wanaojitambua na kufuata misingi ya kiislamu na kijamii.




