Majmaa-Ilmi imeshiriki kwenye ufunguzi wa maonyesho ya Qur’ani kimataifa jijini Tehran

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeshiriki kwenye ufunguzi wa maonyesho ya Qur’ani kimaraifa jijini Tehran.

Rais wa kituo cha miradi ya Qur’ni chini ya Majmaa Sayyid Hasanain Halo amesema “Ujumbe wa Majmaa-Ilimi umeshiriki kwenye hafla ya ufunguzi wa maonyesho ya Qur’ani kimataifa jijini Tehran kwa kuonyesha mafanikio yao ya kielimu”.

Akaongeza kuwa “Ushiriki wa Majmaa-Ilmi katika awamu zilizopita ulikua na muitikio mkubwa kutoka kwa watu waliotembelea maonyesho hayo”.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu hushiriki kwenye maonyesho mbalimbali ya Qur’ani tukufu kwa lengo la kutangaza utamaduni wa kufuata mafundisho ya kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa matabaka tofauti ya jamii na kuboresha uelewa na Dini na misingi ya kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: