Kamati ya kuhuisha turathi imekamilisha semina ya Fiqhi

Kamati ya kuhuisha turathi katika Atabatu Abbasiyya imekamilisha semina ya Fiqhi kwa wanafunzi wa Dini na watafiti.

Semina imeratibiwa na Maahadi ya turathi chini ya kamati, ikiwa ni sehemu ya harakazi zake katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Semina imefundisha mada nyingi, miongoni mwa mada hizo ni: Umuhimu wa Fiqhi, Ufafanuzi wake, Kuanzishwa kwake, Historia yake, Vigawanyo vya Fiqhi vinavyo tambulika katika madhehebu.

Semina ilikua na mihadhara mingi kutoka kwa Sayyid Ali Shahristani, ndani ya siku zote tano za mwanzo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maahadi imeandaa ratiba maalum ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, inahusisha vipengele vya turahi, utamaduni na Dini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: