Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) asubuhi ya Ijumaa ya kwanza katika mwezi wa Ramadhani, umeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru waliokuja kusoma Dua Nudba.
Dua hiyo tukufu imesomwa katika mazingira tulivu, kukiwa na ushiriki mkubwa wa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Watumishi wa Atabatu Abbasiyya huandaa mazingira mazuri kwa ajili ya tukio hilo la kiibada na hutoa huduma za lazima kwa mazuwaru.



