Rais wa kamati ya malezi na elimu amekagua maendeleo ya kazi katika majengo mapya ya chuo kikuu cha Al-Ameed

Rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, Dokta Abbasi Didah Mussawi, amekagua maendeleo ya kazi katika majengo mapya ya chuo kikuu cha Al-Ameed.

Ametembelea majengo hayo akiwa pamoja na mkuu wa chuo Dokta Judat Nuri Aljash’ami na baadhi ya walimu na watumishi wa idara mbalimbali.

Ziara hiyo imelenga kuangalia kiwango cha ukamilifu kwenye majengo mapya na kupata maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi.

Ujenzi wa majengo mapya ya chuo cha Al-Ameed ni sehemu ya kuboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: