Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya inafanya vikao vya usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi wa bweni katika chuo kikuu cha Al-Ameed.
Vikao hivyo ni sehemu ya harakati za idara katika mwezi wa Ramadhani, zinazohudhuriwa na idadi kubwa ya wanafunzi.
Vikao vinapambwa na ratiba tofauti, kunausomaji wa Qur’ani, maelekezo ya kidini kuhusu changamoto mbalimbali, kujadili changamoto za wanafunzi katika uwanja wa kazi baada ya kuhitimu masomo yao, ili kuwajenga kidini na kijamii.
Vikao vinapata ushiriki mkubwa kutoka kwa wanafunzi, kwa lengo la kunufaika zaidi na ratiba ya kila siku yenye vipengele vya kielimu na kidini.



