Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inasoma khitma 60 za Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani, kisomo hicho kinafanywa katika maeneo tofauti ya wilaya kwa lengo la kusambaza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii.
Kiongozi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya Majmaa, Sayyid Haamid Mar’abi amesema, “Tawi la Maahadi linaendesha usomaji wa Qur’ani kwenye maeneo tofauti, idadi ya khitima imefika 60, zikiwemo 3 kuu, kwa ushiriki wa wasomaji 200.
Akasisitiza kuwa “Maahadi inalenga kufika kwenye maeneo yote ya wilaya na kuongeza idadi ya khitma ukilinganisha na mwaka jana, sambamba na kuratibu harakati zingine na nadwa zinazohusu Qur’ani”.
Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu inalenga kujenga misingi bora ya kiislamu katika jamii, na kuongeza uelewa wa kitamaduni na kidini kwa raia wa Iraq.





