Idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya inasoma Qur’ani tukufu ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kiongozi wa idara hiyo, Bibi Adhraa Shami amesema, “Toka mwanzo wa mwezi huu mtukufu tumekua tukisoma Qur’ani kwenye maeneo tofauti ndani ya mkoa wa Karbala, ikiwa ni pamoja na ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amehimiza ulazima wa kusoma Qur’ani katika mwezi huu mtukufu na kutafakari aya zake”.
Akaongeza kuwa “Hafla za usomaji wa Qur’ani zinafungamana na vipengele vingi, kama vile mashindano ya kusoma Qur’ani, masomo ya Fiqhi kwa kubainisha baadhi ya hukumu za Dini, usomaji wa dua za mwezi wa Ramadhani, utoaji wa mihadhara ya kidini, kuhuisha matukio ya kihistoria yanayohusu Ahlulbait (a.s) ndani ya mwezi wa Ramadhani sambamba na kuhuisha siku tukufu za Lailatul-Qadri”.







