Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wameweka mabango meusi ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Bibi Khadija (a.s).
Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu, wameweka muonekano mweusi na mabango yanayo ashiria huzuni yaliyodariziwa maneno maalum ya kuomboleza kifo cha Bibi Khadija (a.s), kama sehemu ya kumuenzi Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kukumbuka kazi kubwa aliyofanya Bibi Khadija (a.s) ya kulinda Dini tukufu ya kiislamu.
Mabango hayo yamewekwa ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo yanayozunguka sehemu hiyo takatifu.
Uandaaji wa mabango na vitambaa umefanywa na idara ya ushonaji na kudarizi chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Ataba tukufu.
Atabatu Abbasiyya inaomboleza kifo cha Bibi Khadija (a.s) kwa kuweka ratiba maalumu, inahusisha ufanyaji wa majlisi za kuomboleza, kutoa mawaidha na kueleza historia ya Bibi Khadija (a.s).





