Idara ya Dini tawi la wanawake inafanya mashindano kuhusu historia ya Bibi Khadija (a.s)

Idara ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imeandaa shindano kuhusu historia ya Bibi Khadija (a.s) wakati wa kuomboleza kumbukumbu ya kifo chake.

Kiongozi wa idara ya habari na harakati Bibi Rajaa Ali Mahadi amesema “Watumishi wa idara wameandaa shindano la kitamaduni kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kuhusu historia ya Bibi Khadija (a.s) sambamba na kuomboleza kumbukumbu ya kifo chake.

Akaongeza kuwa “Shindano linalenga kuangazia nafasi ya Bibi Khadija (a.s) na kutambulisha utukufu wake katika uislamu, bila kusahau namna alivyo jitolea katika kunusuru Uislamu, hakika yeye ni kigezo chema kwa wanawake wote katika msimamo, Imani na kujitolea”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: