Kitengo cha habari na utamaduni kimeandaa program ya “Sallatul-Kaafil” ya kusaidia wanafunzi wa kiafrika katika mwezi wa Ramadhani

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa program iitwayo (Sallatul-Kaafil) ya kusaidia wanafunzi wa kiafrika ndani ya mwezi wa Ramadhani katika mji wa Najafu na Karbala.

Program inasimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo.

Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Shimri amesema “Program ya Sallatul-Kaafil inalenga kusaidia wanafunzi na familia zao katika mwezi wa Ramadhani, mwezi wa rahmah”.

Akaongeza kuwa “Zaidi ya vikapu vya chakula 250 vimetolewa kwa wanafunzi wa Hauza waishio Najafu na Karbala kupitia program hiyo”.

Wanafunzi wameshukuru Ataba tukufu kwa msaada huo wa kibinaadam, wakasema kuwa msaada huo unaimarisha uhusiano na kuwatia moyo wa kuendelea na masomo.

Program hiyo ni sehemu ya huduma za kibinaadamu zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya katika kujenga misingi ya kibinaadamu na kuimarisha undugu na watu wa mataifa tofauti wanaoishi hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: