Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa kikao elimu kupitia ratiba ya mwezi wa Ramadhani.
Kikao kimepambwa na muhadhara wenye anuani isemayo (Kwa namna gani unaweza kuacha athari nzuri), imewasilishwa na Manaal Daakhil, ameongea kuhusu mbinu za kuongea na lugha ya mwili katika mawalisiano.
Hali kadhalika kulikuwa na kipengele kisemacho (wakati picha inapo ongea), amefafanua nafasi ya picha katika kufikisha ujumbe na kutoa uwelewa bila kutumia maneno.
Kituo cha utamaduni wa familia kifananya harakati za kujenga uelewa katika jamii, sambamba na kufundisha mwenendo wa Ahlulbait (a.s), ambao ndio kigezo chema kwa wanaadamu, ili kumfanya mwanaadamu aweze kuacha athari njema na kutengeneza jamii inayo jitambua.