Usomaji wa Qur’ani katika mwezi ya Ramadhani, unaofanywa na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya jijini Baghdad, umeshirikisha walimu wa Vyuo vikuu vya Iraq.
Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Baghdad chini ya Majmaa Sayyid Nabiil Saaidi amesema “Hakika usomaji wa Qur’ani unaoendelea katika mji wa Baghdad, unahusisha watu tofauti katika jamii, kama vile walimu wa vyuo vikuu, wanafunzi wa Dini, vijana na wengineo, kwa lengo la kufikisha ujumbe kuwa Qur’ani ndio njia ya uongofu kwa makundi yote katika jamii, wala sio kundi moja”.
Akaongeza kuwa “Usomaji wa Qur’ani umepata muitikio mkubwa kutoka kwa waumini, hakika kunamazingira mazuri kiimani katika kusikiliza usomwaji wa aya za Qur’ani zinazosomwa kwa sauti nzuri mwezi mzima wa Ramadhani”.








