Mji mtukufu wa Karbala umeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru waliokuja kuhuisha usiku wa Ijumaa ya tatu katika mwezi wa Ramadhani mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mji wa Karbala hupokea idadi kubwa ya watu wanaokuja kufanya ziara kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) siku zote za mwezi mtukufu wa Ramadhani hususan katika siku za Lailatul-Qadri na maombolezo ya kifo cha kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s), ambao huhuisha utiifu wao kwa Ahlulbait (a.s).
Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka mkakati maalum wa kuhudumia mazuwaru na kutimiza mahitaji yao katika siku zote za mwezi mtukufu wa Ramadhani.