Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya semina ya (Mkakati wa kubadili tabia) kwa wanafunzi wake wenye alama za juu.
Semina imefanywa kwa kushirikiana na kitengo cha malezi na elimu katika Ataba tukufu.
Kiongozi wa Maahadi Bibi Manaar Aljaburi amesema “Siku ya kwanza imekuwa na vipengele vingi vinavyo lenga kuwaandaa na hatua ya masomo yenye anuani isemayo (Mkakati wa kubadili tabia za wanafunzi) mada zimewasilishwa na Ustadh Ali Karim Abdu na Falahu Hassan Juma”.
Akaongeza kuwa “Semina itadumu kwa muda wa wiki mbili, nayo ni sehemu ya mradi wa kujenga uwezo wa kiutendaji kwa walimu wa Maahadi, ili waendane na mazingira ya sasa kielimu na kimalezi”.


