Makundi ya mazuwaru wanaomboleza kifo cha Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) mbele ya malalo yake katika mkoa wa Najafu.
Mji wa Najafu umeshuhudia makundi makubwa ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, waliokuja kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini (a.s) na kufanya ibada za usiku wa Lailatul-Qadri.
Mazuwaru huhuisha tukio hilo kwa kusoma dua maalum, ikiwemo dua ya kunyanyua misahafu, kusoma Qur’ani na kufanya majlisi za kuomboleza.










