Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, ameshiriki futari pamoja na watumishi wa kitengo cha kulinda nidham na amepongeza kazi nzuri inayofanywa na watumishi hao katika kuhudumia mazuwaru.
Katibu mkuu amepokewa na rais wa kitengo Sayyid Hussein Shahristani na msaidizi wake pamoja na baadhi ya watumishi.
Sayyid Aalu Dhiyaau-Dini amesema “Ziara hii inatokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, alitutaka kuangalia utendaji wa vitengo vya Ataba tukufu katika kuhudumia mazuwaru, na kutatua changamoto zinazojitokeza katika utoaji wa huduma kwa lengo la kuboresha huduma kwa mazuwaru”.
Akaongeza kuwa “Katika ziara hii tumeshiriki futari pamoja na watumishi wa kitengo cha kulinda nidham, ikiwa kama sehemu ya kutambua kazi kubwa wanayofanya ya kuhudumia mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kulinda nidham ndani na nje ya Ataba tukufu”.
Kitengo cha kulinda nidham kinatekeleza wajibu wake ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo yanayo zunguka sehemu hiyo, kwa kuweka mazingira mazuri kwa mazuwaru hususan wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu.




