Mji mtukufu wa Karbala, umeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru waliokuja kuhuisha usimu wa Ijumaa ya mwisho katika mwezi wa Ramadhani mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mji wa Karbala umepokea idadi kubwa ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, ambao wamekuja kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku wa Ijumaa ya mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Atabatu Abbasiyya imeandaa utaratibu maalum wa kuhudumia mazuwaru na kukidhi mahitaji yao ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.