Majmaa-Ilmi imekhitimisha mashindano ya Qur’ani katika mwezi wa Ramadhani kwa Tartiil katika mkoa wa Dhiqaar

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imehitimisha ratiba ya mashindano ya Qur’ani kwa Tartiil katika mkoa wa Dhiqaar.

Mashindano yameratibiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Dhiqaar chini ya Majmaa, yalikuwa na washiriki 16 kutoka wilaya na vitongoji tofauti, ikiwemo Rifaai, Soko la wazee, Jabaishi, Fadhilah, Batwihaa na Nasiriyya.

Shindano limeendeshwa na jopo la majaji waliobobea katika fani za usomaji wa Qur’ani.

Mashindano ya Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani, ni sehemu ya harakati za Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Dhiqaar ambayo huhusisha wasomaji kutoka maeneo tofauti ya mkoa huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: