Majmaa-Ilmi inagawa zaidi ya sahani za futari 350 kwa mazuwaru kila siku

Majmaa-Ilmi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inagawa zaidi ya sahani 350 za futari kila siku kwa mazuwaru ndani ya mwezi wa Ramadhani.

Kiongozi wa idara ya makaribisho katika Majmaa, Sayyid Alaa Hassan Hashim amesema, Tunatoa huduma mbalimbali ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ikiwemo kugawa zaidi ya sahani za futari 350 kila siku kwa mazuwaru wanaokuja Karbala kupitia barabara ya (Baabil – Karbala) na sehemu zingine sambamba na kutoa huduma zingine.

Akaongeza kuwa, watumishi wa Majmaa kwa kushirikiana na vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu wanatoa huduma bora kwa mazuwaru.

Akafafanua kuwa, Majmaa iliweka mkakati maalum wa kuhudumia mazuwaru katika mwezi wa Ramadhani, na kuwapatia mahitaji yote muhimu ndani ya mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: