Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake imefanya shindano la Qur’ani (kisa cha aya) awamu ya tano.

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefanya shindano la Qur’ani (kisa cha aya) awamu ya tano.

Kiongozi wa Maahadi Bibi Manaar Aljaburi amesema, shindano lilikuwa na washiriki 26 waliohifadhi Qur’ani tukufu, kutoka mkoa wa Najafu, wameshindana katika kueleza madhumuni na visa vya aya za Qur’ani tukufu.

Akabainisha kuwa, Hili ni shindano muhimu kwa waliohifandi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, kwani limejikita katika kutambua maana na visa vya Aya tukufu za Qur’ani.

Shindano la (kisa cha aya) linafanywa kwa mwaka wa tano mfululizo, chini ya ratiba ya Maahadi katika mwezi wa Ramadhani wenye harakati tofauti, linalenga kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani tukufu katika jamii ya wanawake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: