Chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya.. Imeswaliwa swala ya Idi nchini Ujerumani kwa ushiriki wa kundi kubwa la waumini

Kwa usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, imeswaliwa swala ya Idul-Fitri katika mji wa Gottigen nchini Ujerumani kwa ushiriki wa kundi kubwa la waumini.

Muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya katika nchi za Ulaya Sayyid Ahmadi Radhi amesema “Swala ya Idul-Fitri imeswaliwa katika kituo cha Imamu Ridhwa (a.s) mjini Gottigen Ujerumani kwa ushiriki wa idadi kubwa ya waumini”.

Akaongeza kuwa “Kila mwaka swala hii huswaliwa chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, sambamba na kufanya ibada zingine ikiwemo kuandaa futari ya pamoja”.

Atabatu Abbasiyya husimamia harakati mbalimbali za kidini na kitamaduni katika nchi tofauti za ulaya, kwa lengo la kusambaza ujumbe halisi wa kiislamu na utamaduni wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: