Ukumbi wa maonyesho ya makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya umeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru.
Mazuwaru wanakuja kwa wingi katika makumbusho ya Alkafeel kuangalia mali kale ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu tukufu ya Idul-Fitri.
Ukumbi wa makumbusho umepangiliwa vizuri na malikale zimetunzwa kwa umaridadi mkubwa.
Makumbusho ya Alkafeel katika Ataba tukufu, ni moja ya makumbusho bora katika ulimwengu wa kiislamu na inahazina kubwa ya malikale.








