Rais wa kitengo hicho, Sayyid Nasoro Hussein Mut’ibu amesema “Viwanja vya ukanda wa kijani vimeshuhudia idadi kubwa ya familia za wairaq kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala katika siku za Idul-Fitri”.
Akaongeza kuwa Ataba tukufu imeweka mahitaji yote ya lazima sambamba na kuboresha mazingira kwa mapumziko ya wanafamilia katika eneo hilo tulivu.
Familia zimeipongeza Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuboresha mradi wa kijani kibichi na kuwa sehemu bora ya mapumziko kwa wanafamilia.
Mradi wa kijani kibichi ni sehemu bura kwa mapumziko ya wanafamilia, hupokea familia za watu wa Karbala na mikoa mingine wakati wa sikukuu, huandaa mazingira mazuri na rafiki sambamba na kuweka huduma zote muhimu.













