Maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya yanasafishwa baada ya kumaliza siku za kusherehekea Idul-Fitri na ziara ya usiku wa Ijumaa.
Kazi hiyo imefanywa na wahudumu wa kitengo cha utumishi na wahudumu wa uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu.
Kazi imehusisha kusafisha mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), maeneo yanayozunguka Ataba, uwanja wa katikati ya haram mbili, baadhi ya njia zinazoelekea kwenye malalo takatifu na kuondoa taka zote zilizopo kwenye matanki ya taka pamoja na kuyaosha, ili kuhakikisha usafi wa mazingira kwa mazuwaru.
Kazi ya usafi ni endelevu katika Atabatu Abbasiyya, baada ya sikukuu ya Idul-Fitri na usiku wa Ijumaa ya kwanza katika mwezi wa Shawwal, umefanywa usafi mkubwa wa maeneo yote, ili kuweka mazingira mazuri kwa mazuwaru.
Atabatu Abbasiyya tukufu ilipokea makundi makubwa ya watu waliokuja kufanya ziara na kusherehekea sikukuu ya Idul-Fitri.