Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua mlango wa usajili wa kufanyiwa ziara kwa niaba katika makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s) katika mji wa Madina kufuatia kumbukizi ya kuomboleza kuvunjwa kwa makaburi hayo.
Idara ya mitandao chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza ushiriki wa wahudumu wake katika kufanya ziara kwa niaba ya watakaojisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba uliopo katika mtandao wa kimataifa Alkafeel. Unaweza kupakua App ya Alkafeel kwa simu ganja yako yenye (Android) au (ios).
Katika tukio hili wahudumu wa kujitolea miongoni mwa wadau wa ukurasa watafanya ziara na kuswali rakaa mbili kwa nia ya kukidhi haja na kurahisisha mambo kwa niaba ya watu wote watakaojisajili.
