Ataba mbili tukufu zinaomboleza tukio la kuvunjwa kwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s)

Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zinaomboleza tukio la kuvunjwa kwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s).

Hayo yamesemwa katika muhadhara uliotolewa na Sayyid Adnani Jalukhani Mussawi katika uombolezaji wa kumbukumbu ya kuvunjwa kwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s), mbele ya viongozi wa Ataba mbili, wawakilishi wa mawakibu, viongozi wa vikundi vya Husseiniyya na kundi la mazuwaru na waombolezaji wa tukio hilo.

Jalukhani amesema “Kutokea sehemu hii takatifu, tunatoa pole kwa imamu wa zama (a.f), Maraajii wetu watukufu na Maimamu watakasifu kwa kumbukumbu chungu ya kuvunjwa kwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s), tunainua mikono yetu na kuomba dua kwa Mwenyezi Mungu awawezeshe waumini kujenga tena makaburi hayo”.

Akaongeza kuwa “Miongoni mwa kuthibitisha mapenzi kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), ni kufuata mwenendo wao na kutembelea makaburi yao matukufu”, akabainisha kuwa, “Kuvunja makaburi ya Maimamu wa Baqii sio uvunjaji wa mawe na milango tu, bali ni kuonyesha uadui dhidi ya Mwenyezi Mungu mtukufu, aliyetuamrisha kutukuza nyumba za Mitume, Maimamu na watu wema”.

Akaendelea kusema “Utukufu wa Ahlulbait (a.s) na nyumba zao ni mkubwa, kutukuza nyumba kuna wakati inamaana ya kujenga na kunawakati inamaana ya kuheshimu, uvunjaji wa makaburi ya Baqii na Maimamu wawili Askariyaini (a.s) ni kuonyesha kuzidharau sheria za Mwenyezi Mungu, kitabu chake na usia wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: