Wahudumu wa idara ya shamba boy ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya wamepamba majengo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq.
Mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq (Juu ya muongozo wa mwezi awamu ya tano), idara ya mahusiano ya shule chini ya kitengo cha mahusiano cha Ataba tukufu na kauli mbiu isemayo (Kutoka Karbala unamea utoaji) ikiwa ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel na ushiriki wa wanafunzi elfu 5 kutoka vyuo 64 vya mikoa tofauti hapa Iraq.
Wahudumu wa shamba boy wameweka miti na maua kwa mpangilio mzuri katika majengo yaliyopo barabara ya (Najafu – Karbala), kwenye kituo kikuu cha kupokea wanafunzi kwa namna ambayo inaendana na mahafali hiyo.
Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya mahafali hii kwa lengo la kuwatia moyo wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq kutoka mikoa tofauti, na kuwafanya wahitimishe safari yao ya masomo mbele ya malalo takatifu.










