Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya muhadhara wa kuomboleza kifo cha Hamza bun Abdulmutwalib (r.a).
Muhadhara umefanywa ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na umetolewa na rais wa kitengo Shekhe Swalahu Karbalai mbele ya kundi la waumini.
Ameeleza athari ya Ammi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Hamza bun Abdulmutwalib (r.a) na ushujaa wake, amefafanua historia ya maisha yake na nafasi yake katika nyoyo za waumini, bila kusahau kujitolea kwake katika kuuhami uislamu.
Atabatu Abbasiyya huzingatia kuhuisha matukio ya kidini, ikiwa ni pamoja na kuomboleza kifo cha Hamza bun Abdulmutwalib (r.a).