Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya kinafanya semina kwa watumishi yenye anuani isemayo (Mifumo ya idara za kisasa).
Kiongozi wa idara ya mafunzo na mkufunzi Dokta Farasi Shimri, amesema semina itadumu kwa muda wa siku tatu, itakuwa na mihadhara ya msingi ifuatayo: Kutambua mifumo ya idara za kisasa, mbinu za uongozi wenye mafanikio, uundaji wa vikosikazi, uandaaji wa mpango mkakati, utunzaji wa muda, mbinu za mawasiliano, mbinu za kutatua changamoto na kufanya maamuzi.
Semina inalenga kujenga uwezo wa kiutendaji katika idara na kuimarisha uwezo wa watumishi, jambo ambalo linaboresha utendaji wa taasisi za Atabatu Abbasiyya.
Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu hufanya semina na warsha mbalimbali, kwa lengo la kuboresha utendaji wa watumishi wa Ataba tukufu.







