Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka mapambo meusi katika kumbukizi ya kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s)

Wahudumu wa kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wameweka mapambo meusi yanayo ashiria huzuni kufuatia kumbukizi ya kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s).

Rais wa kitengo hicho Sayyid Khaliil Mahadi Hanun amesema “Wahudumu wa kitengo wameweka mapambo meusi yanayo ashiria huzuni, yaliyodariziwa maneno maalum ya kuomboleza kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s) na kuweka muonekano wa huzuni sehemu yote inayozunguka Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Ataba tukufu imepandisha bendera ya huzuni katika eneo la mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na majlisi za kuomboleza zinafanywa ndani ya haram tukufu, kama sehemu ya kumbukizi ya msiba huu mkubwa na kujikumbusha historia ya Imamu Jafari Swadiq (a.s)”.

Atabatu Abbasiyya tukufu huadhimisha matukio yote yanayohusu Ahlulbait (a.s), na kutambulisha elimu zao na misimamo yao katika kutumikia Dini na jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: