Muheshimiwa Sayyid Swafi amesema: Sayyid Ahmadi Ishkuri ni hoja kwa kila mwanafunzi katika umri wake Ikhlasi na juhudi zake

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesema kuwa, Sayyid Ahmadi Ishkuri ni hoja kwa wanafunzi wote katika umri wake, Ikhlasi na juhudi zake.

Ameyasema hayo katika tamasha la kupongeza uandishi wa vitabu vya Imamiyya, vikiwemo vilivyo andikwa na Sayyid Ahmadi Husseini Ishkuri na kuhakikiwa na idara ya maarifa chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya na kauli mbiu isemayo (Chemchem mbili zinazofurika).

Akasema: “Hakika Sayyid Ahmadi Ishkuri ni hoja kwa wanafunzi wote katika umri wake Ikhlasi na juhudi zake, anafundisha, anasoma, anaandika na kufanya uhakiki, kama walivyosema waliotangulia”.

Akaongeza kuwa “Hakika ni hoja hoja kwa kila mwanafunzi, anatakiwa asipoteze muda, siku huisha haraka, (Thamani ya kila mtu hutokana na mema anayoyafanya), pongezi kubwa ziende kwa muheshimiwa kutokana na kazi kubwa aliyofanya na utiifu wake kwa Mwenyezi Mungu, hongera kwa familia yake tukufu”.

Akaendelea kusema “Tunamuomba Mwenyezi Mungu arefushe umri wake na familia yake, awape umri mrefu wahudhuriaji wote, nawashukuru wote mlioshiriki, kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu, rehema na Amani ziwe juu ya Mtume Muhammad na kizazi chake kitakatifu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: