Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani, imekamilisha semina ya kuhifadhi na kusoma surat (Yaasin) kwa wahadhiri wa Mimbari-Husseiniyya.
Semina imehusisha mtihani wa kuhifadhi sura hiyo tukufu na ufasaha katika usomaji kwa kuzingatia hukumu za tajwiid, mbele ya jopo la majaji, washiriki wamefundishwa usomaji wa Qur’ani, kuhifadhi na Fiqhi.
Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani, imeandaa program inayolenga kumjenga mwanamke kielimu, sambamba na kujikita katika kumuwezesha kuwa mtendaji muhimu katika jamii.



