Majmaa-Ilmi imewapa zawadi washiriki wa semina za kufuta ujinga katika chuo kikuu cha Karbala

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imewapa zawadi washiriki wa semina za kufuta ujinga katika chuo kikuu cha Karbala.

Zowezi hilo limefanywa mbele ya rais wa Majmaa-Ilmi Dokta Mushtaqu Ali kwenye hafla ya usomaji wa Qur’ani, iliyoandaliwa na kitivo cha elimu ya kiislamu katika chuo kikuu cha Karbala, ikiwa ni sehemu ya semina ya kufuta ujinga.

Katika ujumbe wake amehimiza kutafuta elimu, kwani ndio msingi wa kuitambua Qur’ani kitabu kitabu kinacho ongoa wanaotaka kuongoka, kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu kimeelekeza maisha mema yenye mafanikio ya kudumu.

Utoaji wa zawadi kwa wanafunzi ni sehemu ya kuwashajihisha kuendelea na masomo, kupongeza juhudi zao, kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani, kufanyia kazi mafundisho yake na kuimarisha Imani katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: