Muheshimiwa Sayyid Swafi amekagua huduma zinazotolewa na kituo cha Ummul-Banina (a.s) na ameelekeza kisaidiwe na kupanua huduma zake kwa mayatima

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amekagua huduma zinazotolewa na kituo cha Ummul-Banina (a.s) katika tiba ya meno, ambacho kinatoa huduma bure kwa mayatima na masikini.

Amekutana na uongozi wa kituo hicho na kusikiliza maelezo yao kuhusu huduma wanazotoa toka kuanzishwa kwake mwana 2013 hadi mwezi wa pili mwaka huu, kimeshahudumia watoto yatima elfu 12, watoto kutoka familia masikini 1100 na watoto 1000 kutoka shule ya Al-Ameed na Alqamaru, huku jumla ya watoto waliofika kwenye kituo kwa ajili ya huduma wakiwa elfu 22.

Muheshimiwa Sayyid Swafi akahimiza kuongeza juhudi na kuhakikisha huduma hiyo inawafikia mayatima wengi zaidi.

Akaelekeza vitengo vinavyofanya kazi na kitengo cha Ummul-Banina (a.s) ndani ya Ataba tukufu visaidie kupanua huduma kwa makundi mengine yenye uhitaji.

Idadi ya madaktari wanaojitolea katika kituo cha Ummul-Banina (a.s) imefika 700, wanatoa huduma kwa mayatima kutoka mikoa tofauti hapa nchini, chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: