Ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) asubuhi ya Ijumaa umeshuhudia kundi kubwa la mazuwaru waliokuja kusoma Dua Nudba.
Usomaji wa dua umefanywa katika mazingira tulivu na kwa ushiriki wa kundi kubwa la mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Wahudumu wa Atabatu Abbasiyya huandaa mazingira mazuri ya usomaji wa dua, kwa kuweka vitabu vya dua, kuandaa sehemu maalum ya kufanyia ibada na kuweka mahitaji ya lazima kwa mazuwaru.





