Atabatu Abbasiyya imekamilisha ratiba ya wiki ya warsha kwa watumishi

Kamati ya program katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imekamilisha ratiba ya wiki ya warsha kwa watumishi.

Ratiba hiyo inasimamiwa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Ataba tukufu, hufanywa kwa muda wa siku tano katika kila wiki.

Ratiba inavipengele vingi, ikiwemo utoaji wa mafunzo mbalimbali, mihadhara ya kielimu, matembezi ya utambulisho na mapumziko kwenye miradi mbalimbali ya Ataba tukufu, ikiwemo kufanya ziara katika malalo ya Imamu Ali (a.s) na kutembelea Maraajii-Dini katika mji wa Najafu.

Ratiba hiyo hufanywa kila wakati, inalenga kujenga uwezo wa watumishi na kuimarisha mawasiliano baina yao.

Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya kila iwezalo katika kujenga uwezo wa watumishi wake, ili kuboresha utoaji wa huduma mbalimbali kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: