Kiongozi wa idara ya kitengo Sayyid Abbasi Ali amesema “Watumishi wa kitengo wamefanya ukarabati wa kiwanda cha barafu, katika sehemu ya kutengenezea na kutunzia barafu, bomba za maji (RO), ikiwa ni katika kujiandaa na msimu wa kiangazi utakaokuwa na ziara inayohudhuriwa na mamilioni ya watu, hususana katika mwezi wa Muharam na Safar”.
Akaongeza kuwa “Kiwanda cha barafu kilicho chini ya kitengo hiki, kinauweza wa kutengeneza barafu 300 kwa saa, ambazo hutolewa bure kwa mawakibu Husseiniyya na wananchi”.
Akasema kuwa “Barafu zinazobaki hutunzwa sehemu maalum, kila sehemu inauwezo wa kuingiza mifuko ya barafu 800 na kwa kiwango cha nyuzi joto 50 chini ya sifuri”.











