Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amehimiza kujali fani zinazo onesha historia na utamaduni wa Iraq.
Ameyasema hayo alipo mpokea mchoraji na mtaalamu wa maumbo, Sayyid Abduridhwa Ali Muhammad kutoka mkoa wa Basra, anaejulikana kwa kazi nyingi alizofanya na kuweka nakshi kwenye aya za Qur’ani katika husseiniyya, miskiti na maeneo mengine.
Muheshimiwa Sayyid Swafi akahimiza kuendeleza ubunifu wa mambo ya kitaifa ili kuonesha utamaduni na kulinda historia ya taifa.
Akasema kuwa “Wasanii wananafasi kubwa ya kuonesha turathi na utamaduni wa taifa kupitia kazi zao, jambo ambalo linasaidia kurithisha vizazi vijavyo”.
Sayyid Abduridhwa Ali Muhammad akasema, Amekutana na Muheshimiwa Sayyid Swafi na kumuambia kuhusu kazi zake, akaeleza lengo lake la kufanya maoneshe ya kazi za mapambo yanayohusu Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya sambamba na turathi za Basra.


