Kituo cha afya na usalama Alkafeel kimetoa mafunzo ya uokozi na huduma ya kwanza katika Atabatu Askariyya

Kituo cha Afya na usalama Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa mafunzo ya uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza kwa watumishi wa Atabatu Askariyya.

Mafunzo hayo yametolewa kwa watumishi wa idara ya uuguzi katika Atabatu Askariyya chini ya program iitwayo (katika kila nyumba muokozi), kwa lengo la kuandaa wahudumu wa afya wenye uwezo wa kutoa huduma za uokozi na huduma ya kwanza kwa haraka wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, hususana wakati wa kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) katika kipindi chote cha mwaka.

Semina imedumu kwa muda wa siku nne, kila siku ilikuwa na mihadhara miwili, zimeongelewa mada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na namna ya kuamiliana na watu wenye matatizo ya moyo, watoto wadogo na matatizo ya kuvunjika viungo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: