Atabatu Abbasiyya imeweka muonekano wa furaha kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Ridhwa (a.s)

Kitengo cha kusimamiwa haram katika Atabatu Abbasiyya kimeweka mapambo yanayoashiria furaha kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Ridhwa (a.s).

Mabango yameshonwa na idara ya ushonaji na kudarizi chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Ataba tukufu.

Wameweka maua na mabango ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), yaliyoandikwa maneno mazuri ya pongezi za kuadhimisha mazazi ya Imamu Ridhwa (a.s).

Uwekaji wa mapambo hayo ni sehemu ya mkakati maalum wa kupokea mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaokuja kuadhimisha tukio hilo tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: